Loading...

MAENEO/SHUGHULI ZA MRADI

Mradi huu utajikita kuwezesha vijana kwenye kilimo cha mbogamboga kama vile kabeji, pilipili hoho, nyanya na vitunguu maji kwa kutumia umwagiliaji wa matone. UTEKELEZAJI WA MRADI Mradi huu utatekelezwa kama ifuatavyo; 1. Kutoa mafunzo kwa vijana kumi (10) watakao kuwa wawezeshaji kwa vijana wengine. 2. Kutoa mafunzo ya ujasiliamali katika kilimo 3. Kutoa mafunzo ya vitendo kwa vijana arobaini (40) kuhusu kilimo cha umwagiliaji na namna ya kuandaa mifumo ya umwagiliaji 4. Kuunda mtandao wa vijana wanaojishughulisha na kilimo cha umwagiliaji 5. Kuanzisha shamba darasa la kilimo cha umwagiliaji 6. Kuwakutanisha wakulima vijana na wadau ambao ni Taasisi za fedha, Wauzaji wa pembejeo za kilimo na Wafanyabiashara watumiaji wa mazao ya bustani.